Balozi Yakubu, hii ndiyo Comoro

  Na Ahmed Rajab   UHUSIANO baina ya Tanzania na Comoro unatazamiwa kupaa na kukua baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Saidi Yakubu kuwa balozi mpya wa nchi yake visiwani Comoro.  Yakubu aliyehitimu shahada ya sheria nchini Uingereza kabla ya kurudi Tanzania na kufanya kazi bungeni na baadaye kuwa katibu mkuu katika wizara ya […]

Tafakuri za ghafla juu ya Muungano

  Na Ahmed Rajab   KUTIMU miaka 60 ya Muungano wa Tanzania mnamo 26 Aprili, 2024, kumezidi kuwasisimua na kuwatia jazba baadhi ya waumini wa Umajumui wa Afrika. Mhemuko wao umewafanya wausukume na wajaribu kuufikisha mbinguni Muungano huo. Wanauelezea kuwa ni mfano thabiti wa umoja halisi wa Afrika.     Mashabiki hao wa Muungano wanasisitiza […]

Tafsiri ya “Sauti ya Dhiki”: Ushairi kama silaha ya ukombozi

Na Ahmed Rajab   Sura ya nje ya kitabu cha Mtazamo wa Kifikra wa “Sauti ya Dhiki” ya Abdilatif Abdalla.  Mashairi yamefasiriwa kwa Kiingereza na Ken Walibora Waliaula na kitabu kizima kimehaririwa na Annmarie Drury. Kitabu hicho chenye kurasa 344 kimechapishwa na University of Michigan Press na Afrika kimechapishwa na Mkuki na Nyota Publishers, Dar […]

Tunafuturu futari, hatufutari futuru

  Na Ahmed Rajab   MIAKA kadhaa iliyopita katika siku kama hizi za mfungo wa Ramadhani niliwahi kuandika makala katika gazeti la Raia Mwema ambamo nililalama jinsi aina kwa aina ya mapishi asilia ya Kiswahili yalivyotoweka Zanzibar baada ya Mapinduzi ya 1964.     Nilijawa na furaha nilipoona kwamba makala hayo yaliwachochea wengine kuendeleza na […]

TAABINI YA MZEE ALI HASSAN MWINYI

TAABINI Ali Hassan Mwinyi “Mzee Rukhsa”: (Mei 8,1925 – Februari 29, 2024) Mtu wa watu aliyependwa na masharifu ALHAJI Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki dunia Dar es Salaam, Alhamisi iliyopita, siku 70 kabla ya kutimia miaka 99, aliushangaza ulimwengu alipoibuka kuwa Rais wa tatu wa Zanzibar 1984. Mwinyi aliushangaza tena ulimwengu miezi kadhaa baadaye alipochomoza kuwa […]

Afrika Kusini ilicheza na shingo ilitoa

Picha: Mmoja wa waandamanaji akifurahia hukumu ya Mahakama ya Haki ya Kimataifa (ICJ) dhidi ya Israel jijini The Hague hivi karibuni. Picha kwa hisani ya Foreign Policy   Na Ahmed Rajab   ISRAEL haina uso.  Inajaribu kujikaza kisabuni na kujitoa kimasomaso lakini Mahakama ya Kimataifa (ICJ), mjini Hague, Uholanzi, yameiumbua kwa unyama inaoufanya dhidi ya […]

Afrika katika mkorogo wa vita vya Gaza

Rais Joe Biden akiwa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Picha ya Shirika la AP   Na Ahmed Rajab   ZAIDI ya siku mia zimekwishapita tangu majeshi ya Israel yaanze kulitwanga eneo zima la Ukanda wa Gaza, ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi mashambulio yakushangaza dhidi ya Israel yaliyofanywa na Mvuvumko wa Muqawama wa […]

“Ujutar” wa kisiasa na kuporomoka kwa demokrasia

Picha: Rais Donald Trump. Picha kwa hisani ya mtandao wa AP.   Na Ahmed Rajab   SITOSHANGAA ukinambia hujui “ujutar” ni nini au “jutar” ni nani.  Niliwauliza watu kadhaa wa sehemu mbalimbali za Uswahilini na wapo walionambia hawajawahi kuzisikia kalima hizo mbili.   Nimechungulia kwenye makamusi mawili matatu ya Kiswahili humo namo sikuyaona.   Hata […]

Wakati Kissinger alivyomlazia Nyerere

Rais Julius Nyerere akiwa na Henry Kissinger jijini Dar es Salaam mwaka 1976. Picha kwa Hisani ya Cambridge University Press   Na Ahmed Rajab   DAKTA Henry Kissinger aliyefariki dunia Kent, Connecticut, Marekani, Novemba 29 mwaka huu alikuwa mwingi wa mengi.  Alikuwa msomi wa hali ya juu, gwiji wa diplomasia, mshauri wa siasa za kimataifa […]

Waisraeli wanaiogopa hata furaha ya Wapalestina

Picha kwa Hisani ya Pars Today Na Ahmed Rajab KISWAHILI chetu hakina neno moja lenye tafsiri ya neno la Kiingereza ‘resistance.’ Lakini lugha za Kiarabu na Kifarsi (Kiajemi), ambazo tumezoea kuazima misamiati yao, zote zinalo neno moja lenye maana ya ‘resistance.’ Na lugha zote hizo mbili zinalitumia neno hilo hilo moja lililoanzia kwenye Kiarabu: ‘muqawama.’ […]