Senegal: Funzo kubwa zaidi ni wapinzani kuaminiana

Rais Macky Sall wa Senegal akiwatembeza Rais mteule wa Senegal, Diomaye Faye (kushoto kwake) na Ousmane Sonko (kulia kwake)  kwenye Ikulu ya Dakar hivi karibuni. Picha kutoka mtandao wa Quest France.   Na Zitto Kabwe   Mtandao wa Viongozi wa Upinzani katika Bara la Afrika (Pan African Opposition Leaders Solidarity Network) umepoteza wanachama wake wawili […]

IWD: Ushiriki wa siasa usisubiri nyakati za uchaguzi pekee

Na Fortunata Kitokesya   SIKU ya Kimataifa ya Wanawake Duniani (International Women’s Day) ina mchango mkubwa kwa usawa na haki za wanawake wote duniani. Ni siku muhimu ya kutambua mapambano endelevu ya usawa wa kijinsia na kusherehekea mafanikio ya wanawake ulimwenguni kote.   Pia ni siku ambapo watu binafsi, mashirika, na jamii wanakusanyika kwa pamoja […]

Aina tano za UONGO wa ubeberu, ukweli mmoja wa umma

Picha: Mmoja wa waandamanaji barani Ulaya akiwa ameshika bango linalotaka majeshi ya Israel yasitishe mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina hivi karibuni. Picha kwa hisani ya mtandao wa Forward.   Na Issa Shivji   KUNA mtu aitwaye Joseph Goebbels aliyekuwa Waziri wa Propaganda katika utawala wa fashisti Adolf Hitler. Goebbels aliwahi kusema ukirudiarudia uongo hatimaye […]

Kavazi la Dkt. Salim: Jenerali Ulimwengu na Gazeti la Rai mwaka 1995

Na Mohamed Said KATIKA Kavazi la Dk. Salim Ahmed Salim anaeleza simu aliyopigiwa na Jenerali Ulimwengu tarehe 29 Machi 1995 na walizungumza kuhusu Burundi, siasa za Tanzania na Uchaguzi Mkuu wa mwaka huo. Mimi nilivutiwa na hili la Uchaguzi Mkuu wa 1995 kwa kuwa kwa njia moja au nyingine nilihusika na nilikuwa kama alivyokuwa akifanya […]

Pitio la Kitabu: ‘’Survived and Thriving cha Madiha Tubman

Picha: Ukurasa wa mbele wa kitabu cha Survived and Thriving. Picha kwa hisani ya Mohamed Said   Na Mohamed Said   KUANZIA  mwanzo wa kitabu ukurasa wa kwanza akili yako itakuambia kuwa mkononi kwako umeshika kitabu ambacho si cha kawaida; si kitabu utakachosoma na kikombe cha kahawa mkononi.   Kitabu kinaanza katika hali ya vita […]

Mkama Ndume na ukarimu wa Wapemba

Picha: Mwandishi wa makala haya, Mohamed Said, akishiriki chakula na wenyeji wake kisiwani Pemba hivi karibuni. Picha kwa hisani ya Mohamed Said   Na Mohamed Said     Wenyeji wangu wananitembeza kila sehemu Pemba. Ndani ya gari yetu kumetiwa maji ya kunywa, majamvi na viti vya kukunja ikiwa vitahitajika. Maji ya kunywa kuchukuliwa nimeelewa ila […]

Ni nguvu ya kisiasa au nguvu ya rushwa?  

Picha: Wananchi wa Afrika Kusini wakiandamana kupinga vitendo vya rushwa vinavyofanywa na viongozi wa kisiasa wa taifa hilo.   Na Godfrey Dilunga   ILIKUWA mwaka 1962, jijini Dar es Salaam, Rais Julius Nyerere, wakati huo, alifungua Mkutano wa Vijana Duniani. Katika hotuba yake ya ufunguzi iliyopewa jina la The Second Scramble, alitetea ujamaa akisema utajiri […]