Kosa la Freeman Mbowe

  Na Ezekiel Kamwaga     MWAKA 2015, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilipata mafanikio makubwa katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania. Kilipata takribani asilimia 40 ya kura zote zilizopigwa – kiwango ambacho kilikuwa hakijawahi kufikiwa na chama chochote cha upinzani katika historia ya taifa letu.     Kulikuwa na mambo mawili katika ushindi huo […]

Kosa la Tundu Lissu

Picha kwa Hisani ya Gazeti la Citizen la Tanzania   Na Ezekiel Kamwaga   MARA nyingi ninapofanya uchambuzi kuhusu wanasiasa, huwa ninaamini kuwa kuna wanasiasa wa aina tatu; wanasiasa wa kipekee, wanasiasa wa kitaasisi na wanasiasa wa msimu.   Wanasiasa wa kipekee ni wale ambao si wa kawaida. Nazungumzia watu wa aina ya Nelson Mandela […]

Ancien Regime, Abdul Nondo na watu kutekwa

  Na Ezekiel Kamwaga     KATIKA uchambuzi wake wa nini kilisababisha Mapinduzi ya Ufaransa ya mwaka 1789, Alexis du Tocqueville aliandika kitu cha tofauti na wengine walioandika kuhusu mapinduzi yale. Alisema mapinduzi yale hayakuwa tukio la mara moja bali ni hitimisho la miaka mingi ya kuharibika kwa mfumo wa utawala wa taifa hilo.   […]

Rais Samia wa G20

MAELEZO YA PICHA: Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo ya uwili (bilateral)  na Rais wa Indonesia, Prabowo Subianto, pembezoni mwa mkutano wa G20 uliofanyika Rio de Janeiro, Brazil, wiki iliyopita.   Na Ezekiel Kamwaga   MOJAWAPO ya taswira zilizobaki kwenye kumbukumbu zangu kuhusu Mkutano wa Nchi Tajiri Duniani maarufu kwa jina la G20 uliomalizika […]

Ajali ya Kariakoo, angani na Rio: Saa 15 za kwanza

  Na Ezekiel Kamwaga   DAKIKA chache baada ya ndege iliyombeba Rais Samia Suluhu Hassan kupaa angani kwenda Brazil kuhudhuria mkutano aliopewa heshima ya kualikwa wa Nchi Tajiri Duniani wa G20, habari zilianza kusambaa mitandaoni kuhusu kuanguka kwa jengo la biashara katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.   Kwa bahati nzuri, ndani ya […]

Septemba 23 isiwe maafa, uwe mwanzo mpya

  Na Ezekiel Kamwaga   KESHO, Septemba 23, 2024, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepanga kufanya maandamano hapa nchini kupinga vitendo vya utekaji na mauaji vinavyoonekana kukithiri hapa nchini hivi sasa.   Mpaka wakati naandika makala haya, ninafahamu kwamba CHADEMA wameamua kesho watafanya maandamano hayo. Na mpaka wakati huu, Polisi hawajatoa taarifa yoyote kuruhusu […]

Chawa ni nani?

Tajiri Elon Musk wa Marekani (kushoto) katika picha na mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump. Picha kwa hisani ya IBTimesUK     Na Ezekiel Kamwaga     KWA wafuatiliaji wa siasa za Marekani kuelekea uchaguzi wao wa Novemba mwaka huu, watakuwa wamebaini namna Elon Musk; mmoja wa matajiri wakubwa duniani, anavyomuunga mkono mgombea […]

Babu Duni na binti yangu: Somo la Unyenyekevu  

  Na Ezekiel Kamwaga   SIKU moja majira ya saa tano usiku, nilipokea simu kutoka kwa mwanasiasa mkongwe wa Zanzibar, Juma Duni Haji. Alikuwa ananipigia kwa vile hakupokea wakati alipopigiwa simu kutoka kwangu saa kadhaa nyuma.   Nilipoiona tu nilitabasamu maana nilijua kilichotokea. Sikuwa nimempigia mimi isipokuwa binti yangu mwenye umri wa miaka mitatu wakati […]

January, uwaziri na mengine

    Na Ezekiel Kamwaga   KATIKA kipindi cha takribani miaka 60 ya nchi yetu – na pengine duniani kwa ujumla, P mbili; Perfomance and Politics (Siasa na Utendaji), zimeamua uwepo wa waziri au mawaziri kwenye Baraza la Mawaziri.   Rais anaweza kumbadili au kubadili mawaziri kwa sababu ya utendaji wao mbovu au kwa sababu […]

Tanzania Tower: Idan na Picha kubwa

Mwonekano wa majengo pacha ya Tanzania Tower mara yatakapokamilika   Na Ezekiel Kamwaga   MAPEMA mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Nje, January Makamba, alipokea simu kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Serikali ya Nigeria kuhusu suala la kiwanja ambacho Tanzania ilipewa katika eneo zuri la Lagos takribani miaka 34 iliyopita lakini hadi sasa hakuna […]