Balozi Yakubu, hii ndiyo Comoro

  Na Ahmed Rajab   UHUSIANO baina ya Tanzania na Comoro unatazamiwa kupaa na kukua baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Saidi Yakubu kuwa balozi mpya wa nchi yake visiwani Comoro.  Yakubu aliyehitimu shahada ya sheria nchini Uingereza kabla ya kurudi Tanzania na kufanya kazi bungeni na baadaye kuwa katibu mkuu katika wizara ya […]

Siku January alipokutana na Wang Yi

Na Ezekiel Kamwaga   MWAKA jana, marais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Xi Jin Ping wa China walifanya mabadiliko katika mabaraza yao ya mawaziri na kuwapa nafasi wanasiasa wawili ambao ndiyo wasaidizi wao wakuu kwenye masuala ya diplomasia na uhusiano wa kimataifa.   Julai mwaka 2023, Rais Xi alimteua mwanadiplomasia mbobezi, Wang Yi, kuwa […]

Chapo tayari, Tanzania icheze kete ya kwanza

Na Ezekiel Kamwaga   MAPEMA kabisa, ni muhimu nikaweka wazi kwa nini naandika uchambuzi huu. Kwanza Msumbiji ni rafiki wa damu wa Tanzania, pili kwenye mpaka wetu nao kuna tishio la kiusalama na tatu tunapakana katika eneo ambako huenda nchi yetu ikafanya mradi mkubwa zaidi wa uwekezaji kwenye historia yake – wa LNG. Ni nchi […]

Tafakuri za ghafla juu ya Muungano

  Na Ahmed Rajab   KUTIMU miaka 60 ya Muungano wa Tanzania mnamo 26 Aprili, 2024, kumezidi kuwasisimua na kuwatia jazba baadhi ya waumini wa Umajumui wa Afrika. Mhemuko wao umewafanya wausukume na wajaribu kuufikisha mbinguni Muungano huo. Wanauelezea kuwa ni mfano thabiti wa umoja halisi wa Afrika.     Mashabiki hao wa Muungano wanasisitiza […]

Tafsiri ya “Sauti ya Dhiki”: Ushairi kama silaha ya ukombozi

Na Ahmed Rajab   Sura ya nje ya kitabu cha Mtazamo wa Kifikra wa “Sauti ya Dhiki” ya Abdilatif Abdalla.  Mashairi yamefasiriwa kwa Kiingereza na Ken Walibora Waliaula na kitabu kizima kimehaririwa na Annmarie Drury. Kitabu hicho chenye kurasa 344 kimechapishwa na University of Michigan Press na Afrika kimechapishwa na Mkuki na Nyota Publishers, Dar […]

Kraken ameachiwa

Na Ezekiel Kamwaga KATIKA  filamu maarufu ya Clash of the Titans ya mwaka 2010, Liam Neeson – akiigiza kama mungu wa hekaya  za Kigiriki Zeus, alitamka maneno “Release the Kraken”. Kraken ni lidubwana lisilo na huruma ambalo Zeus aliagiza lifungiwe baharini, chini ya ulinzi wa Poseidon – mtawala wa baharini kwenye hekaya hizohizo, ili asidhuru […]

Mrithi wa Makonda: CCM na revolvere  

  Na Ezekiel Kamwaga   NI kazi ngumu kubashiri uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, kwenye nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho. Ukiangalia waliochukua nafasi hiyo kabla, huwezi kutunga uzi au shanga kuunganisha matukio.   Hakuna sababu ya waziwazi ya kusema kwa nini alimpa nafasi kwanza Shaka Hamdu […]

Kujenga au kubomoa si usanii, ni siasa

  Na Ezekiel Kamwaga   KUNA uhusiano wowote kati ya siasa na majengo? Kuna uhusiano wowote baina ya viongozi na matukio ya kujenga au kubomoa vitu? Jibu langu ni ndiyo na makala yangu hii itaeleza juu ya mifano na namna kujenga au kubomoa kunavyoweza kumjenga mwanasiasa au utawala mbele ya wananchi wake.   Ninaandika makala […]

Tunafuturu futari, hatufutari futuru

  Na Ahmed Rajab   MIAKA kadhaa iliyopita katika siku kama hizi za mfungo wa Ramadhani niliwahi kuandika makala katika gazeti la Raia Mwema ambamo nililalama jinsi aina kwa aina ya mapishi asilia ya Kiswahili yalivyotoweka Zanzibar baada ya Mapinduzi ya 1964.     Nilijawa na furaha nilipoona kwamba makala hayo yaliwachochea wengine kuendeleza na […]

Senegal: Funzo kubwa zaidi ni wapinzani kuaminiana

Rais Macky Sall wa Senegal akiwatembeza Rais mteule wa Senegal, Diomaye Faye (kushoto kwake) na Ousmane Sonko (kulia kwake)  kwenye Ikulu ya Dakar hivi karibuni. Picha kutoka mtandao wa Quest France.   Na Zitto Kabwe   Mtandao wa Viongozi wa Upinzani katika Bara la Afrika (Pan African Opposition Leaders Solidarity Network) umepoteza wanachama wake wawili […]