Tanzania flag waving against cloudy sky

Miaka 30 ya Vyama Vingi: Changamoto na Mustakabali kusonga mbele

LEO Tanzania inatimiza miaka 30 tangu turejee rasmi katika siasa za mfumo wa vyama vingi. Katika kipindi hicho, taifa letu limepitia katika kipindi cha furaha, majonzi, misukusuko na changamoto zote wakati taifa linapoanza njia mpya. Jambo hili si jepesi kwa sababu nyakati hizo hazikuwa rahisi duniani kote.