Mtihani wa Rais Samia na Waziri Ummy

Na Ezekiel Kamwaga   MWISHONI mwa wiki hii, nilikuwa na mjadala mzuri katika mojawapo ya makundi sogozi niliyopo. Rafiki yangu mmoja alijenga hoja kwamba tatizo la akinamama kujifungulia sakafuni lililotawala sana katika vyombo vya habari na mitandaoni hapa nchini au mwenendo wa suala la Naibu Waziri wa zamani wa Sheria na Katiba, Pauline Gekul, yasingetokea […]

Lamata: Taa ya Tamthilia za Nyumbani

Na Ezekiel Kamwaga MWAKA 2017 alijitambulisha kupitia tamthilia ya Kapuni iliyorushwa na kituo cha DSTV. Tangu wakati huo, Leah Richard Mwendamseke, amekuwa akifyatua tamthilia ambazo zimekuwa sehemu ya maisha ya Watanzania – sasa akitamba na ile ya Jua Kali. Kwa wengi, Mwendamseke ni alama ya tamthilia za Kitanzania na safari yake haikuwa rahisi. Yeye ni […]

Teri: Tanzania ya Uwekezaji

Na Ezekiel Kamwaga NAMBA zinazungumza kuliko maneno. Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan, alimteua Gilead Teri, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Wakati anapewa nafasi hiyo, wastani wa miradi ya uwekezaji iliyokuwa inarekodiwa na kituo hicho kwa miaka mitatu ya nyuma ilikuwa takribani 56. Katika mwaka wake wa kwanza tu, […]

Mkenda: Mageuzi ya Elimu

Na Ezekiel Kamwaga INGAWA kitaaluma ni mchumi, Profesa Adolf Mkenda, amejipambanua katika mwaka huu kama mwanasiasa anayetaka kuona mabadiliko kwenye sekta ya elimu ili iendane na changamoto za kisasa nchini na kimataifa. Kuanzia mwakani, Wizara ya Elimu imeandaa mitaala mipya ambayo itawafanya wahitimu kuwa na maarifa zaidi na uwezo mkubwa zaidi wa kukabili changamoto za […]

Karia: Rais wa Mpira

Na Ezekiel Kamwaga MWAKA 2023 umeshuhudia Tanzania ikipewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yaliyopangwa kufanyika mnamo mwaka 2027. Tanzania itaandaa mashindano hayo kwa ushirikiano wa pamoja kati yake na jirani zake wa Kenya na Uganda. Hata hivyo, hakuna shaka kwamba Tanzania ndiyo hasa ilifanikisha ushindi […]

January: Alama kila anapoenda

Na Ezekiel Kamwaga MFANO mmoja unatosha kumueleza Waziri wa Mambo ya Nje, January Makamba, na utendaji wake tangu alipoingia kwenye wizara hiyo mwaka huu. Kwenye ndege wakati tukirejea Dar es Salaam kutoka India kwenye ziara ya kitaifa ya Rais Samia nchini humo, mmoja wa mawaziri alinieleza kwamba tangu awe waziri – ziara ile ilikuwa ndiyo […]

Zitto: Kaka wa Maridhiano

Na Ezekiel Kamwaga MWANZONI mwa mwaka huu, Kiongozi wa Chama wa  ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, alikuwa pengine mwanasiasa aliyekuwa akishambuliwa zaidi mitandaoni kuliko mwingine. Mashambulizi hayo yalitokana na ushiriki wake katika Kikosi Kazi kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mapitio ya sheria za uchaguzi zilizopo nchini. Kikosi kazi hicho hakikuwa kinaungwa mkono na chama […]

Hussein Bashe: Kilimo ni dili

Na Ezekiel Kamwaga SIKU moja tukiwa New Delhi, India, kwenye ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, alifanya mkutano na waandishi wa habari wa Tanzania tuliokuwa pale. Nakumbuka alipomaliza mkutano, nilikwenda kumshika mkono na kumkumbatia, nikamueleza kwamba nimefurahi kwa kilichotokea. Bashe alikuwa ametoka kueleza waandishi wa habari kuhusu makubaliano ya Tanzania […]

Prof. Janabi: Jeshi la Mtu Mmoja

Na Ezekiel Kamwaga MAJUZI nilihudhuria harusi moja jijini Dar es Salaam na wakati muda wa kwenda kula ulipofika, MC akatania “wakati tunapokwenda kupakua chakula, msisahau ushauri wa Profesa Janabi”. Ukumbi mzima ulilipuka kwa vicheko. Ni kama kila mtu alikuwa anamjua Profesa Mohamed Janabi na ujumbe wake kwa jamii yake. Kwa hakika, katika mwaka 2023, hakuna […]

“Ujutar” wa kisiasa na kuporomoka kwa demokrasia

Picha: Rais Donald Trump. Picha kwa hisani ya mtandao wa AP.   Na Ahmed Rajab   SITOSHANGAA ukinambia hujui “ujutar” ni nini au “jutar” ni nani.  Niliwauliza watu kadhaa wa sehemu mbalimbali za Uswahilini na wapo walionambia hawajawahi kuzisikia kalima hizo mbili.   Nimechungulia kwenye makamusi mawili matatu ya Kiswahili humo namo sikuyaona.   Hata […]