Mkenda: Mageuzi ya Elimu

Na Ezekiel Kamwaga

INGAWA kitaaluma ni mchumi, Profesa Adolf Mkenda, amejipambanua katika mwaka huu kama mwanasiasa anayetaka kuona mabadiliko kwenye sekta ya elimu ili iendane na changamoto za kisasa nchini na kimataifa.

Kuanzia mwakani, Wizara ya Elimu imeandaa mitaala mipya ambayo itawafanya wahitimu kuwa na maarifa zaidi na uwezo mkubwa zaidi wa kukabili changamoto za kimaisha za kisasa ikiwemo elimu ya ufundi stadi. Mojawapo ya mabadiliko makubwa itakuwa ni kufanya elimu ya msingi kuwa miaka sita badala ya sasa huku ile ya awali ikiwa miaka miwili.

Kama msomi, Mkenda anafahamu ubaya wa kuongoza taifa lenye wasomi wasiopikwa kukabili changamoto za kisasa na bila shaka miaka mingi baada ya uwaziri wake, faida za mawazo yake ya kimageuzi zitaonekana kwa watoto na wajukuu zetu.