Nyakati za Samia na Hakainde

Na Ezekiel Kamwaga   Katika moja ya hotuba zake maarufu za zamani, Baba wa Taifa la Zambia, Dk. Kenneth Kaunda, alipata kuelezea uhusiano baina ya taifa lake na Tanzania kuwa sawa na ule wa pacha walioungana. Hakuna kilichokuwa kinaeleza uhusiano huo kama uhusiano baina yake na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.   Wawili hawa […]

Namna Rais Samia ‘alivyoiteka’ India

  Na Ezekiel Kamwaga   NIANZE kwa kutumia takwimu kueleza kile nilichopanga kuandika kwenye makala haya.   Katika siku nne ambazo Rais Samia Suluhu Hassan alikaa nchini India, Oktoba 8 mpaka 11 mwaka huu, kuna siku mbili ambazo jina lake liliongoza kwa kusakwa kupitia mitandaoni na raia wa taifa hilo.   Siku ya kwanza ilikuwa […]

Nyerere na namna ya kudhibiti Jeshi

Na Ezekiel Kamwaga   RAIS Yoweri Museveni wa Uganda alipata kuulizwa wakati mmoja kuwa ni jambo gani kubwa analodhani Baba wa Taifa la Tanzania, Julius Nyerere, alilifanya kiasi cha kubaki madarakani kwa muda mrefu? Pasi na kufikiri sana, Museveni alijibu; “He tamed the army” Kwa tafsiri ya haraka ya lugha ya Kiswahili, alimaanisha alilidhibiti Jeshi. […]

Ya Dk. Salim: Namuelewa Mzee Warioba, lakini….  

Picha: Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere akiwa na Dk. Salim   Na Ezekiel Kamwaga   KWENYE tukio la uzinduzi wa Makavazi ya Dk. Salim Ahmed Salim jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Profesa Said Yahya Othman aliuliza swali gumu kwa wazungumzaji watatu katika tukio lile; kuhusu ubaguzi ulio wazi katika siasa za Tanzania.   Kama […]

TANESCO: Nyamo-Hanga, Ulanga, Makamba na wahanga

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa tukio la kuapisha mabalozi na watendaji wengine wa serikali lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam wiki hii. Picha ya Ikulu     Na Ezekiel Kamwaga   KUELEWA uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kumfanya Boniface Gissima Nyamo-Hanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la TANESCO kunahitaji tafakuri ya mambo […]

“Baba yenu ni Doto, Uwaziri umekuja na utaondoka”

Picha: Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko (kulia), akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, katika mojawapo ya matukio ya kiserikali hivi karibuni.   Na Ezekiel Kamwaga   DESEMBA 30, mwaka 1978, mapacha walizaliwa katika familia moja ya wakulima huko Bukombe. Wazazi hawakuwa na uwezo wa kuhudumia mapacha hao peke yao huku wakiendelea […]

Sheikh Abbas Idi, pumzika kwa amani Janat Firdaus

Picha: Sehemu ya umati wa wananchi  waliojitokeza kwenye mazishi ya Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Kigoma, Abbas Idi Noboka, Agosti 29, 2023. Picha kwa hisani ya Zitto Kabwe.    Na Zitto Kabwe   Sheikh Abbas Idi Noboka, Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Kigoma, Mjumbe wa Baraza la Masheikh Mkoa na Sheikh wa Kata ya Mwanga […]

Nyerere alivyomtetea Karume Accra

Picha: Sheikh Vuai Kitoweo, aliyekuwa Rais wa Chama cha Hizbu. Picha kwa hisani ya Ahmed Rajab   Na Ahmed Rajab   KATIKA mwezi wa Machi hali ya hewa jijini Accra, Ghana, huwa inaudhi bila ya kiasi kwa joto linavyokuwa kali. Jioni ndipo huzidi kushtadi.  Nadra mvua kunyesha.     Siku moja Machi 1958, saa za […]

Kachero Siwa, Kadari na Siasa za TISS

Rais Samia Suluhu Hassan akimwapisha Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wiki hii. Picha kwa Hisani ya Ikulu     Na Ezekiel Kamwaga     MARAIS huwa hawachagui siku au mazingira yatakayowafanya washike wadhifa huo katika wakati husika. Kama ungekutana na Ali Hassan Mwinyi mwaka 1983 na kumueleza […]

Kadinali Pengo angesemaje kuhusu Waraka wa Maaskofu?

  Na Ezekiel Kamwaga   KUELEKEA kipindi cha Kwaresma na Sikukuu ya Pasaka ya mwaka 2018, Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC) lilitoa waraka ambao kimsingi ulikosoa vitendo vya uminyaji wa demokrasia na uhuru wa watu kujieleza uliokuwepo wakati wa utawala wa hayati Rais John Magufuli.   Waraka ule ulikuwa na sehemu nne lakini […]